Home Habari Haji Manara: Niliwaambia hamkusikia

Haji Manara: Niliwaambia hamkusikia

2 min read
0
0
Baadhi ya viongozi wa Simba wakiwa furaha zilizojaa furaha baada ya kuchukua ubingwa wao.

Afisa habari wa Mabingwa wa Ngao ya Jamii, Simba SC, Haji Manara amefunguka kwa kuwapiga dongo watani wao Yanga kwa kuwaambia ametimiza yale aliyowaahidi ya kuwafunga mabao matano bila ya kujalisha aina ipi ya ufungaji.

Manara ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ulipomalizika mtanange wa kukata na shoka na hatimaye timu ya Simba kuibuka washindi kwa mikwaju ya penati 5-4 baada ya kumaliza dakika 90 za mchezo kwa sare ya bila ya kufungana.

“Niliwaambia tutawafunga ‘khamsa’ haijalishi kwa vipi. Haya nendeni mkalale sasa”, aliandika Manara.

Baadhi ya viongozi wa Simba wakiwa furaha zilizojaa furaha baada ya kuchukua ubingwa wao.
Kutokana na ushindi huo walioupata timu ya wekundu Msimbazi ni ishara tosha ya kuwajuza wadau na wapenda soka kutambua kwamba msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara umeshaanza kwa mwaka 2017/2018.

Katika hatua nyingine, Nahodha wa Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga, Haroub Cannavaro amewapongeza vijana wake kwa kuonyesha mchezo mzuri pamoja na wapinzani wao Simba kwa kuchukua kombe hilo huku akiwapiga dongo kwa kudai matuta ni mchezo wa kubahatisha.

Kwa upande mwingine, msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mwaka 2017/2018 unatarajiwa kuanza Agosti 26 mwaka huu siku ya Jumamosi kwa kuwakutanisha Simba na Ruvu Shooting, Azam FC kucheza na Ndanda FC huku siku ya Jumapili Agosti 27 nayo Yanga itacheza na Lipuli FC

Facebook Comments

Load More Related Articles
Load More By Osward Anderson
Load More In Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Check Also

Mwanamuziki Ali Kiba Atupa Jiwe Gizani

STAA anayekimbiza na Wimbo wa Seduce Me, Ali Kiba Saleh ‘King Kiba’ ametupa jiwe gizani kw…