Home Trending Mtandaoni Gigy Money, Barnaba wafunguka haya baada ya kuambiwa wapenzi

Gigy Money, Barnaba wafunguka haya baada ya kuambiwa wapenzi

1 min read
0
0
Gigy Money
 

BAADA ya Gigy Money na Barnaba  kupiga picha wakiwa wamepakatana na kuzua gumzo kwenye mitandao ya kijamii wakidaiwa kwamba ni wapenzi, Elias Barnaba ‘Barnaba’ na muuza sura Gift Stanford ‘Gigy Money’ wameibuka na kudai kuwa wao si wapenzi.

Awali kulikuwa na nyepesinyepesi zikidai kuwa hiyo haikuwa mara ya kwanza kwa wawili hao kuonekana wakiwa wamepakatana katika maeneo mbalimbali, wakisema baada ya Barnaba kuachana na mkewe, aliamua kujiweka kwa mwanadada huyo asiyeishiwa matukio mjini.

Barnaba.
 

Za Motomoto News ilipowasiliana na Barnaba, alisema Gigy Money ni dada yake kama walivyo madada wengine na katika maisha yake haishi kwa skendo hivyo wanaosema hivyo siyo kweli.

Kwa upande wake Gigy, alisema Barnaba ni kaka yake na pia shemeji yake, kwani ni rafiki wa aliyekuwa mpenzi wake, Mo J na hiyo picha walipigwa wakiwa kwenye shoo hivyo hakuna suala la mapenzi kati yao.

Facebook Comments

Want more stuff like this?

Get the best viral stories straight into your inbox!

Don’t worry we don’t spam

Website design tanzania
Load More Related Articles
Load More By Osward Anderson
Load More In Trending Mtandaoni

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Check Also

Mchumba afungukia mavazi ya Shilole

Zuwena Mohamed. JAMAA ambaye ndiye usingizi wa staa wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed, Ashraf…