Home Habari Wolper: Nitaendelea Kubadiri Wanaume

Wolper: Nitaendelea Kubadiri Wanaume

1 min read
0
1

WAKATI mashabiki wakiwa bado wanamshangaa staa wa Bongo Muvi, Jacqueline Massawe‘Wolper’ juu ya tabia yake ya kubadili wanaume kila kukicha, katika hali ya kushangaza, ameibuka na kudai kuwa ataendelea kubadili wapenzi, muda wowote atakapogundua kuwa aliyenaye, hana vigezo.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko hivi karibuni, Wolper alisema hawezi kuogopa maneno ya watu wanayosema juu yake kwa vile hawaelewi anachokumbana nacho katika mapenzi, kwani hawezi kung’ang’ania kukaa kwenye uhusiano ambao haendani nao au unampa shida.

“Unajua unapokuwa na mpenzi huwezi kujua kuna tabia utakumbana nazo ambazo haziendani na wewe, lakini pindi unapogundua ni bora kuondoka kuliko kukaa sehemu ambayo huna furaha nayo,” alisema Wolper.

Staa huyo aliongeza kuwa hata mtu aliyenaye hivi sasa endapo atagundua kama tabia hazirandani, ataangalia ustaarabu mwingine kwani haogopi kusemwa kuhusu kubadilisha wapenzi.

Facebook Comments

Load More Related Articles
Load More By Salum Milongo
Load More In Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Check Also

Mwanamuziki Ali Kiba Atupa Jiwe Gizani

STAA anayekimbiza na Wimbo wa Seduce Me, Ali Kiba Saleh ‘King Kiba’ ametupa jiwe gizani kw…