Home Habari Kwanini Wema Sepetu hajakabidhiwa kadi ya CHADEMA jana?

Kwanini Wema Sepetu hajakabidhiwa kadi ya CHADEMA jana?

1 min read
0
0

Cherlie Aries

Jana vyombo vya habari vilikua-standby kupokea taarifa za maamuzi rasmi ya Mwigizaji Wema Sepetu ambayo kwenye kutangazwa kwa maamuzi hayo, Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye ambaye sasa ni miongoni mwa viongozi wa CHADEMA ndio alikua msimamizi mkuu.

Mpaka jioni zoezi hilo ambalo lilikua limepangwa kufanyika Magomeni Dar es salaam mbele ya Waandishi wa habari liliahirishwa baada ya Waandishi kumsubiri kwa muda mrefu Wema Sepetu atokee eneo la tukio ambapo Mzee Sumaye alisema yafuatayo >>> “tulitegemea kwamba kesi ya Wema Sepetu ingemalizika mapema Mahakamni ili aje hapa”

“Sababu kubwa ya yeye kuja hapa ilikua ni jambo alilonalo la kuwaeleza Waandishi na pia kubwa alikua anajiunga rasmi na chama cha CHADEMA na mimi kazi yangu ilikua ni kuwapa hizo kadi na wao kuwasalimia na kusema kwanini wameamua kujiunga rasmi”

“Jambo hilo lilikua gumu kutekelezeka kwasababu kesi yake ilichukua muda mrefu Mahakamani kuliko muda tulioutarajia lakini bila shaka litatekelezeka wakati mwingine”

Facebook Comments

Load More Related Articles
Load More By Salum Milongo
Load More In Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Check Also

Mwanamuziki Ali Kiba Atupa Jiwe Gizani

STAA anayekimbiza na Wimbo wa Seduce Me, Ali Kiba Saleh ‘King Kiba’ ametupa jiwe gizani kw…