Home Habari Afungwa Jera Miaka 45 kwa Uporaji

Afungwa Jera Miaka 45 kwa Uporaji

1 min read
0
0

DAR ES SALAAM: Dereva teksi Rashid Yusuph (23) ahukumiwa kifungo cha miaka 45 jela, baada ya kupatikana na hatia ya uporaji wa kutumia nguvu.

Mshtakiwa alikuwa anakabiliwa na mashtaka 3 ya unyang’anyi wa kutumia nguvu dhidi ya raia 3 wa kigeni ambao walikuja nchini kwa ajili ya kufanya utafiti na utalii.

Akisoma huku hiyo, hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, Ritha Tarimo alisema imemtia hatiani mshtakiwa kama alivyoshtakiwa hivyo atatumikia kifungo cha miaka 45 jela ili iwe fundisho.

Hakimu Tarimo alisema ameridishwa na ushahidi wa mashahidi saba waliotoa mahakamani hapo dhidi ya mshtakiwa huyo. “Nakuhukumu kifungo cha miaka 45 jela kwa makosa yote matatu ya unyang’anyi wa kutumia nguvu, kwa sababu tukio hili lilitokea sehemu moja na kwa wakati mmoja hivyo, kila kosa moja utatumikia kifungo cha miaka 15 na adhabu hii ina kwenda kwa pamoja,” alisema Hakimu Tarimo.

Facebook Comments

Load More Related Articles
Load More By Salum Milongo
Load More In Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Check Also

Mwanamuziki Ali Kiba Atupa Jiwe Gizani

STAA anayekimbiza na Wimbo wa Seduce Me, Ali Kiba Saleh ‘King Kiba’ ametupa jiwe gizani kw…