Home Habari Undani Kifo cha Ivan

Undani Kifo cha Ivan

1 min read
0
0

Na Salum Kim Milongo

ALIYEKUWA mume wa Zari Hassan “Zari Boss Lady,”Ivan Ssemwanga “Ivan Don,” amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Steve Biko, Pritoria nchini Afrika Kusini.

Ivan amefariki dunia kwa kile kinachodaiwa ni shambulio la moyo.

Alianza kujihisi vibaya mapema mwanzoni mwa mwezi huu na siku chache kabla ya kifo chake alikimbizwa hospitali ya Steve Biko kwa ajili ya kupata matibabu.

Hali iliendelea kuwa mbaya siku baada ya siku na usiku wa kuamkia mei 25,2017 ndio Ivan alifariki dunia.

Ivan anatajwa kama shujaa na baba wa watoto watatu. Katika siku za uhai wake ametumia muda wake kujiimalisha kiuchumi na kuisaidia jamii yake.

Ivan alikuwa ni bilionea wa Uganda aliyehamishia makazi yake Afrika Kusini mwaka 2002.

Aliwekeza katika elimu Afrika ya Kusini ambapo alifungua Chuo kikuu kilichojulikana kama Bloockliny Colleges chenye matawi katika miji mikubwa kama vile Pretoria, Jobeg na Daben.

 

Facebook Comments

Load More Related Articles
Load More By Salum Milongo
Load More In Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Check Also

Mwanamuziki Ali Kiba Atupa Jiwe Gizani

STAA anayekimbiza na Wimbo wa Seduce Me, Ali Kiba Saleh ‘King Kiba’ ametupa jiwe gizani kw…