Home Hadithi/ Makala “Mjane Mpya” Sehemu ya Kwanza 01

“Mjane Mpya” Sehemu ya Kwanza 01

7 min read
0
2

DEREVA wa daladala ndiye alikuwa mtu wa mwanzo kubaini kuwa kuna abiria amefariki dunia ndani ya gari, alizungumza kwa kinyume na kondakta wake ili abiria wengine wasielewe.
“Amajaa naona riga nzito kuna tum kavuta humu”, alisema dereva akimwambia konda wake.
“Likwe jaa leyu aliyepandia lepa darajani”, konda alimjibu dereva wake huku akiangaza ndani ya gari kubaini kama ni kweli yule aliyekuwa anayemdhania ndiye aliyekufa ama laa.
Dereva kwa hekima akaliegesha gari pembeni ili ashauriane na konda wake nje ya gari, waliposhuka tu abiria waliyokuwa wakiwahi makazini walianza kufoka kwa maneo ya kebehi kuonesha wazi kuidharau kazi ya uchukuzi wa abiria kwa kudaui huduma ni mbovu uswahili.
Ghafla kilisikia kilio ndani ya gari, ni baada ya mke wa Mzee Muzeiya kubaini kuwa mume wake haongei, mwanzo alihisi ni kalala tu kumbe mzee huyo ndio alikuwa ameiaga dunia kwa maradhi yaliyomshambulia kwa majuma mawili mfululizo.
Konda na dereva walirudi haraka ndani ya gari na kuwaomba abiria watulie.
“Jamani kuna mwenzetu ametutoka tukiwa ndani ya gari hatujui ni wapi alikuwa anaelekea lakini akili ya haraka haraka tumebaini kuwa alikuani mgonjwa maana hata wakati anapanda gari alipanda kwa kujikongoja sana na alikuwa akitokwa na mapovu mdomoni”, alisema hivyo konda.
Huzuni iliibuka mara moja kwa abiria wote walimtupia macho mwanamke aliyeukumbatia mwili unaosemekana kufa ukikimbizwa hospitali, hata wale wenye haraka ya kwenda kazini walirudisha mioyo yao nyuma na kutanguliza ubinadamu mbele na utanzania kama ilivyo desturi yetu kusaidiana wakati wa matatizo.
Hakuna hata abairia mmoja aliyeshuka badala yake wote wakausindikiza mwili wa marehemu hospitali ya Amana iliyopo Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam .
Mama mmoja alijitolea kanga yake na mwili wa mzee mzeiya ukafunika kwani wakati anakata roho mapuvu yalimtoka zaidi mdomoni. Mkewe ameshikwa na akina dada wanafunzi wa chuo waliokuwa wanawahi vipindi katika chuo cha habari kilichopo meneo hayo.
Konda alizima wimbo wa shangwe uliokuwa ukipigwa ndani ya gari na muda huo akawakaribisa abiria wenye kuyajua maneno ya imani kuzungumza ndani ya gari.
Abiria wote walionekana kuguna na baada ya sekunde chache alisimama kijana wa makamo na kujitambulisha kwa jina la Alhaji Yusuph Seif.
“Nimesimama hapa si kama muislam bali nimesimama hapa kama mtanzania mwenye hofu ya Mungu, nimeumia sana na tukio lililotokea leo asubuhi ndani ya Gari, siwezi kulaumu kwani ni kazi ya Mungu. Naomba ushirikiano wenu, mimi siwafahamu ndugu hawa waliofiwa ila hali ya huyu mama amenigusa sana naomba tumchangie chochote tulichonacho na mimi nitanunua sanda kwa ajili ya kumsitili ndugu yetu huyu”, alimaliza kwa dua aliyoimba kwa lugha ya Kiswahili na wote waliitikia kana kwamba ni waumini wa dhehebu moja.
Hali ile ya umoja, ilipendeza mno japo ilikuwa ni huzuni sana. Walipofika Ilala Bungoni jirani kabisa na hospitali ya Amana alisimama mchungaji naye alisema machache kuonyesha namna alivyoguswa na tukio lile na aliwapongeza abiria wote kwa ushirikiano walioutoa na alitamani waumini wake wangekuwa kama wale abiria.
Walipofika hospitali, watu maalum waliondaliwa kwa ajili ya kuwapoke wagonjwa na maiti walifanya kazi yao, Mwili wa Mzee Mzeiya ulipelekwa katika chumba maalum cha kuhifadhia wafu na mke wa marehemu alianza kusambaza taarifa kwa nduugu na jamaa wa karibu wa familia wa familia.
Daladala iliondoka na abiria waliendelea na pirika zao za kuwahi makazini, waliobaki pale ni Alhaji Yusuph na Mchungaji ambaye jina lake halikufahamika mara moja. Walipeana mawasiliano na abiria wazalendo wakiahidi kuwajulisha kitakoendelea katika kupanga shughuli za mazishi.
Majira ya saa nne asubuhi Alhaji Yusuph alishangaa ndugu wa marehemu walioanza kuwasili. Walikuwa ni watu wenye uwezo sana na ufakiri wa marehemu mzee Mzeiya na mkewe uliibua maswali mengi sana kwa Alhaji Yusuph na mchungaji waliobaki kumfariji mke wa mzee Mzeiya.
Yaliegeshwa magari ya kifahari yenye namba za serikali na mengine yenye namba maalum za majina ya wamiliki. BMW 6453 iliyoandikwa BLANDINA na Prado iliandikwa SON. Alhaji alishikwa na shauku kutaka kujua wale ni akina nani watu wenye ukwasi mkubwa na ndugu yao afie kwenye daladala?
Itaendelea
Naitwa Salum Kim 0652 262 797

Facebook Comments

Want more stuff like this?

Get the best viral stories straight into your inbox!

Don’t worry we don’t spam

Website design tanzania
Load More Related Articles
Load More By Salum Milongo
Load More In Hadithi/ Makala

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Check Also

Siwezi kumuacha mume wangu ingawa ana VVU.:soma makala hii ya kusisimua.

  “NIMEMPOKEA na kumkubali bila kujali hali yake, nimemuuguza akiwa kwenye hali mbaya hadi…